12 NOVEMBA 2024
MP3•Αρχική οθόνη επεισοδίου
Manage episode 449797549 series 2027789
Το περιεχόμενο παρέχεται από το UN Global Communications (Digital Solutions Unit) and United Nations. Όλο το περιεχόμενο podcast, συμπεριλαμβανομένων των επεισοδίων, των γραφικών και των περιγραφών podcast, μεταφορτώνεται και παρέχεται απευθείας από τον UN Global Communications (Digital Solutions Unit) and United Nations ή τον συνεργάτη της πλατφόρμας podcast. Εάν πιστεύετε ότι κάποιος χρησιμοποιεί το έργο σας που προστατεύεται από πνευματικά δικαιώματα χωρίς την άδειά σας, μπορείτε να ακολουθήσετε τη διαδικασία που περιγράφεται εδώ https://el.player.fm/legal.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Havana Cuba amabpo Flora Nducha amaezungumza na mshiriki kutoka maitaifa mbalimbali na leo ni Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani inayotupeleka Zimbabwe.Kuongeza kiwango cha fedha kwenye ufadhili wa miradi ya kukabili na kuhimili tabianchi nchi ikiwa ni moja ya masuala muhimu yanayojadiliwa katika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP29 huko Baku, Azerbaijan, leo ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema bila kupunguza kwa kiasi kikubwa hewa chafuzi, na kuimarisha miradi ya kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi, kila uchumi duniani utakumbwa na madhara makubwa.Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR iliyotolewa leo huko COP29 inaonesha ni kwa jinsi gani watu wanaokimbia vita, ghasia na mateso wanazidi kujikuta kwenye mazingira yaliyokumbwa na janga la tabianchi, janga ambalo linawaweka kwenye mchanganyiko wa vitisho, lakini bila fedha wala msaada wa kukabiliana navyo.Na mamia ya wakimbizi wanaotaka kujiunga na elimu ya juu sasa watafanya bure mitihani ya kuonesha umahiri wao wa lugha ya kiingereza, au IELTS. Hii inafuatia makubaliano ya ushirikiano kati ya UNHCR na mfumo wa kimataifa wa lugha ya kiingereza, IELTS.Na mashinani COP29 ukiendelea huko Baku Azerbaijan, tunabisha hodi nchini Zimbabwe ambako Umoja wa Mataifa unawasaidia wakulima kakabiliana na mabadiliko ya tabianchi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
…
continue reading
100 επεισόδια